BAADA ya Afrika Kusini kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea, kiungo wa Bafana Bafana, Thabiso Kutumela, amesema matokeo hayo yameibua matumaini makubwa baada ya mchezo wa kwanza kupata sare.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Mandela, Kampala, Uganda, Afrika Kusini walimiliki mpira hadi dakika ya saba walipopata bao kupitia kwa Neo Maema, kabla ya Kutumela kuongeza la pili dakika ya 54.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kutumela, ambaye pia aliibuka na tuzo ya mchezaji bora wa mechi, alisema watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye kundi hili na ushindi wa mechi hiyo umewapa matumaini makubwa.
“Nasikia furaha kushinda tuzo hii, lakini hii tuzo naitoa kwa wachezaji wenzangu, kocha, na wafanyakazi wote wa kiufundi tuliopambana kwa pamoja,” alisema Kutumela na kuongeza:
“Pointi hizi zinatupa morali baada ya sare kwenye mchezo uliopita. Ili kuwa mechi ngumu, tulifunga kisha tukarudi nyuma, jambo ambalo liliigharimu timu bao na kutoa nafasi kwa Guinea kusawazisha.”
Kuhusu umuhimu wa ushindi huo, Kutumela alisema: “Mchezo huu ni muhimu, kila mchezo utakuwa muhimu, na hatuwezi kupoteza pointi hadi tukutane na Uganda na Niger, wapinzani wetu wa mwisho ambao watatuvusha kwenda robo fainali.”
“Tunahitaji kuendelea kuamini hadi mwishoni mwa mechi ya mwisho kwa sababu hakuna kilichopotea bado. Tuna nafasi. Huu ulikuwa ushindi wa kuimarisha morali na tulistahili.”