New Amaan kweupe,  Senegal ikiivaa Congo Brazaville CHAN 2024

Licha ya mashindano ya CHAN kuwa na hadhi ya kimataifa, huku yakishirikisha vipaji vya Ligi za ndani kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Uwanja wa New Amaan unaonekana  kuwa na idadi ndogo ya watazamaji.

Katika hali hiyo,  watetezi Senegal wanatupa tena karata yao ya pili kwenye uwanja huo jioni hii dhidi ya Congo ikiwa ni mechi ya Kundi D. 

Senegal inasaka ushindi wa pili baada ya mechi ya kwanza kuichapa Nigeria, huku Congo wao ikisaka ushindi wa kwanza baada ya kutoka sare mechi ya kwanza dhidi ya Sudan.

Ilikuwa mechi yenye mvutano wa hali ya juu, ambapo kila upande ulitambua uzito wa alama tatu. Senegal itaingia ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Nigeria, huku Congo ikihitaji ushindi baada ya sare yao ya 1-1 na Sudan.

Mechi hii ni  ya kwanza kwa Senegal na Congo kukutana katika historia ya CHAN, licha ya kuwa ni mara ya nne kwa kila taifa kushiriki mashindano haya.

Kwa Senegal, ushindi ulikuwa na maana ya kufuzu moja kwa moja kwa hatua ya robo fainali, lakini kwa Congo, utafanya kundi hilo kuendelea kuwa wazi. Kundi hili lililopangwa Zanzibar linaahirikisha timu nne tofauti na makundi mengine matatu ya A, Bna C yenye timu tano kila moja, huki Tanzania ikiwa ya kwanza kutinga robo kutoka Kundi B.