……………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.
Viongozi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake ya nyongeza ya mishahara, kupandisha madaraja ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya shukrani kutoka kwa Rais wa TUCTA, Bw. Tumaini Nyamhokya kwa kutambua mchango wake katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo, Bw. Tumaini Nyamhokya, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.