Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications, Rosalynne Mndolwa-Mworia ni miongoni mwa mashuhuda wa mchezo wa CHAN 2024 kati ya Burkina Faso dhidi ya Mauritania uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jana Agosti 13, 2025.
Licha ya kushuhudia mchezo huo pia alikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo El Mami Tetah (Mauritania) ambapo Burkina Faso imepoteza kwa bao 1-0.
Rosalynne ametumia fursa hiyo kuwaomba mashabiki wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kujitokeza kwa wingi Kwa Mkapa Agosti 16, 2025, kuipa mzuka Stars ikicheza dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
“Niwakaribishe na wengine waje viwanjani kupata bururdani ya soka, zaidi sana mashabiki wajae kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Taifa Stars, Agosti 16 dhidi ya Afrika ya kati ili kuihamasisha timu yetu ya Taifa kupanda ushindi ifike mbali kwenye mashindano haya”.
Huo utakuwa mchezo wa mwisho kwa Stars ambayo tayari imefuzu hatua ya mtoano wa michuano hiyo kwa kushinda mechi tatu za awali.
Taifa Stars ilianza kwa kuichapa Burkina Faso mabao 2-0 kisha ikaibonda Mauritanian kwa bao 1-0 kisha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar.