Wakati Mbeya City ikiingia rasmi kambini kesho Ijumaa huko Mwakaleli katika mji wa Tukuyu, wilayani Rungwe Mbeya, uongozi wa timu hiyo umesema umeridhishwa na maandalizi na kutamba kufanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Timu hiyo iliyorejea Ligi Kuu baada ya kupotea misimu miwili, imefichua kukamilisha usajili wa wachezaji 27 wakiwamo wa kimataifa.
Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ally Nnunduma amesema usajili walioufanya unaenda kuwapa mafanikio katika kumaliza nafasi saba za juu na kwamba suala la bajeti wamejipanga vyema ndani na nje ya uwanja.
Pia amegusia tukio la Mbeya City Day litakalofanyika Septemba 6, likitanguliwa na uzinduzi wa jezi, Septemba 1, matukio yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini humo.