Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Oryx imezindua kampeni ya Yente kwa Miezi mitatu kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Watanzania ikiwa ni kulinda afya pamoja na mazingira.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Zakhem jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia wa Wizara ya Nishati Nolasco Mlay amesema kuwa Serikali inashirikiana na katika mkakati wa kuhamasisha matumizi Nishati Safi ya Kupikia.
Amesema kuwa kwa mwaka 2025 ni kusambaza mitungi ya gesi zaidi ya 400000 hadi kufikia Juni wamesambaza mitungi 200000 hadi kufikia Desemba dhamira ya Serikali itakuwa imetimia.
Mlay amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati wanaendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Aidha amesema kuwa matumizi ya kuni yanaharibu mazingira pamoja na afya hivyo nia ya Serikali kutaka wananchi wote watumie nishati Safi ya kupikia.
Mkurugenzi wa Oryx Tanzania Benoit Araman amesema kuwa Kampeni hiyo ni pamoja ya kurejesha mitungi ya zamani ambapo mtu akinunua gesi kwa mtungi wa zamani atapewa mtungi unaoenda na muda uliopo hivi sasa.
Amesema kuwa mitungi ya gesi inakuwa na muda baada ya hapo inatakiwa kurejeshwa ambapo kwa sasa katika kampeni hiyo wateja Oryx wataponunua gesi watapata huduma hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa katika kampeni hiyo wateja watapata zawadi kupitia mitungi hiyo watakutana na tarakimu za namba na kutuma na ndipo itajulikana zawadi.
Meneja wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Oryx Shaban Fundi amesema kuwa Oryx imejipanga katika mkakati wa Serikali wa kutumia nishati safi ya kupikia kwa kila mtanzania kufikiwa.