Mkuu wa Mkoa wa Songwe Jabir Omari Makame ametoa amewataka wananchi wa Songwe kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali kuwafichua wote wanaofanya magendo na wanaokwepa kulipa kodi.
Ameyasema hayo leo Agosti 13,.2025 alipokutana na maafisa wa TRA wakiongozwa na Meneja wa TRA mkoa wa Songwe CPA. Rashid Harith waliofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza zoezi la Elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Makame amesema kwa kushirikiana na raia wema pamoja na vyombo vya ulinzi wataendelea kudhibiti magendo yanyaoingizwa nchini ili mipakata ya nchi ibaki kuwa salama na kuwasaidia TRA kukusanya kodi stahiki kwa maendeleo ya Tanzania.
“Naomba tutoe ushirikiano tunopata taariza kwa wanaojihusisha na magendo tuweze kuzifikisha kwa vyombo husika ili kueza kuchukua hatua, ili tuweze kujenga nchi yetu.”
Aidha, amewapongeza TRA kwa kuwafikia wananchi hususan wafanyabiashara kuwapa elimu ya kodi na kuwafundisha mabadiliko ya sheria za kodi huku akiwata wananchi watoe ushirikiano kwa TRA kwa kulipa kodi zao kwa hiari bili ya kushurutishwa kwa kutambua kuwa kodi ndio msingi kuu wa maendeleo ya nchini.
Nitoe wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa TRA na serikali kwa kulipa kodi bila ushuruti kwa kutambua kuwa kulipa kodi maana yake tunaamua aina ya Tanzania tunayoijenga, tunaamua kuboresha huduma za aftya, tunaamua kuboresha elimu, tunamua kuboresha miundo mbinu ya barabara.”
Kwa upande wake, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi, CPA Paul Walalaze amesema TRA kupitia Idara ya Elimu kwa mlipakodi na Mawasiliano imejiwekea utaratibu kuwa kila mwaka mpya wa fedha unapoanza kuwafikia wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuwapatia elimu ya sheria ya fedha ya mwaka 2025 kupitia njia mbalimbali kama vile semina na vipindi vya redio ili waweze kujua mabadiliko ya kodi yaliyomo katika sheria hiyo na waweze kulipa kodi kwa hiari na urahisi zaidi.
“Sisi TRA, kupitia Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano tumekua na utaratibu wa kuwafikia wafanyabiashara na wananchi nchi nzima kwa lengo la kuwafunisha mabadiliko mbalimbali ya kodi yaliyomo katika sheria mpya ya fedha ili waelewa mabadiliko hayo na waweze kulipa kodi kwa usahihi na urahisi”
Akigusia baadhi ya mabadiliko ya kodi yaliyomo amemsema moja ya wapo ya sheria zilizofanyiwa marekebisho ni sheria ya Mapato ambapo ndani yake imetaja mabadiliko ya katika uwasilishaji wa ritani na utozwaji wa kodi kwenye makampuni.
Kwa upande wao wa wafanyabiashara biashara wamefurahia elimu hiyo na kuahidi kuendelea kulipa kodi kwa hiari huku wakitoa wito kwa TRA waendelee kutoa elimu hiyo ili kuwasaidia wao kulipa kodi kwa wakati na kuepukana na changamoto.