DR Congo yaiong’oa Angola CHAN 2024

KIPIGO  cha mabao 2-0 kutoka kwa DR Congo katika pambano la Kundi A la michuano ya CHAN 2024 umeing’oa Angola katika michuano hiyo ikiungana na Nigeria, Afrika ya Kati na Zambia.

DR Congo ilipata ushindi huo kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya katika pambano kali, huku washindi wakipata mabao dakika 45 za pili.

Angola iliyokuwa ikicheza mechi ya nne ya kundi hilo na kuaga ikiwa na pointi nne tu ikiziacha Kenya, Morocco na ĎR Congo.
Timu hii inakuwa ya pili kuaga mashindano katika kundi hilo baada ya Zambia iliyoshindwa kupata japo pointi moja.

Vita kubwa inaonekana kubakia kwa timu tatu zinazoongoza ambazo zote zimebakisha mechi moja mkononi.

Timu hizo tatu zitamaliza hatua ya makundi Agosti 17 ambapo Kenya itakutana na Zambia katika uwanja wa Nyayo, Nairobi kuanzia saa 9:00 alasiri wakati DR Congo ikiumana na Morocco muda sawa lakini zenyewe zitakutana kwenye Uwanja wa Moi Kasarani, Nairobi.

Ikiwa Kenya yenye pointi saba itapoteza kisha Zambia nà DR Congo na Morocco zikatoka sare, ili kuchagua timu mbili zitakazokwenda robo fainali kwa kuangalia tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mabao mawili ya DR Congo yote yalifungwa kipindi cha pili kupitia Jephte Kitambala Bola dakika ya 58 kisha Makonzi Katumbwe akafunga la pili dakika ya 70.