MAMELODI Sundowns ya Afrika Kusini, imetangaza rasmi, kuondoka kwa kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho, Neo Maema.
Matajiri hao wa Sauzi, wamemuaga kiungo huyo leo Ijumaa, baada ya kuitumikia klabu hiyo miaka minne kwa mafanikio.
Hatua ya Maema kupewa ‘Thank you’ ni kama inawashwa taa ya kijani kwa kiungo huyo kutua Simba.
Maema ndani ya Mamelodi ameshinda jumla ya mataji saba, yakiwemo ubingwa wa Ligi Kuu mara nne, Kombe la Nedbank Moja, MTN8 moja na ubingwa wa African Football League.
Kiungo huyo ndani ya miaka minne akiwa Mamelodi amecheza jumla ya michezo 120, akifunga mabao 13, akitengeneza asisti 14.
Kiungo huyo atajiunga na Simba, mara baada ya kumalizika kwa Fainali za Ubingwa wa Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN akiwa tayari ameshafunga bao moja akiwa na kikosi cha Afrika Kusini ambacho ndio nahodha wao.
Kiungo huyo ni chaguo la kocha Fadlu Davids, aliyependekeza usajili wake ndani ya kikosi hicho kilichopo kambini Misri ikijiandaa na msimu mpya wa mashindano.