Wakati Uchaguzi Mkuu wa TFF ukiendelea jijini Tanga, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa shirikisho hilo anayewania Kanda Namba Tatu, Evance Gerald Mgeusa amejiondoa kuwania nafasi hiyo.
Mgeusa alikuwa akigombea nafasi ya Utendaji wa TFF Kanda Namba Tatu, inayohusisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Songea.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Kiomoni Kibamba, amesema mgombea huyo ameamua kujitoa kwa hiari yake Mwenyewe.
“Yupo hapa katika mkutano ila ameamua kujitoa kwa hiari yake mwenyewe na sasa kanda namba tatu imebakia na wagombea wawili pekee,” amesema.
Katika kanda namba tatu, Mgeusa alikuwa akigombea na James Patrick Mhagama na Cyprian Charles Kuyava.