FIFA yaipigia chapuo Mnyanjani soka la vijana

RAIS wa TFF Wallace Karia amesema Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, uliopo Mnyanjani jijini Tanga, umeteuliwa na FIFA kwa lengo la kukuza vipaji vya soka la vijana.

Akizungumza katika hotuba yake baada ya kuidhinishwa na wajumbe wa mkutano mkuu, Karia amesema FIFA imetoa nafasi hiyo kutokana na kuridhishwa na maendeleo yaliyopo.

“Kwa furaha niseme pia FIFA imetupa hadhi kubwa ya uwanja wetu wa Mnyanjani uwe kitovu cha kukuza soka la vijana, hii ni heshima na tunapaswa kujivunia,” amesema Karia.

Aidha Karia amesema kituo hicho kimekuwa ni sehemu ya mafanikio ya soka la vijana hivyo, FIFA haijakosea kutoa nafasi hiyo na heshima kwa Tanzania.