Karia: Chuma kimepita kwenye moto

Rais mteule wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wallace Karia amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi, kwa imani yao kwake.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo uliofanyika jijini Tanga na kushinda kwa kishindo amesema haikuwa rahisi kwa mchakato huo wa uchaguzi.

Karia amewataka wajumbe wa mkutano huo wasiumie na lolote kwani hatua hiyo imekuwa ni sawa na kupitisha chuma kwenye moto ili kiwe imara.

“Misukosuko tuliyopitia ni ishara kwamba tunachangamoto kwa hiyo tunatakiwa kwenda kuzifanyia kazi,”amesema Karia.

“Nawashukuru kwa imani yenu kwangu na wenzangu, kitu tunachotakiwa kufanya sasa ni kila mmoja akafanye kazi yake, tutakwenda kuendelea kusimamia uendeshaji mzuri wa mpira wetu.”