Nyambaya, Lufano nje, Kulunge, Hossea ndani

Uchaguzi wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji umepeleka kilio kwa waliokuwa wajumbe wa Kanda Namba Moja Lameck Nyambaya na namba tano Vedastus Lufano baada ya kuanguka.

Nyambaya ambaye alikuwa anatetea kiti chake ameanguka baada ya kupata kura 33 wakati mshindi akiibuka Hossea Lugano aliyepata kura 40.

Katika uhesabuji wa kura hizo kura tatu ziliharibika, baada ya wapiga kura kuandika namba kwenye karatasi hizo.

Lufano naye ameanguka kwa kupata kura 35 akiangushwa na Salum Kulunge aliyejipatia kura 41 huku kukiwa hakuna kura iliyoharibika

Naye James Mhagama aliyekuwa anagombea Kanda namba tatu licha ya kukauka sauti amefanikiwa kutetea kiti chake akipata kura 47 wakati Cyprian Kuyava akipata kura 27.

Matokeo hayo yanawafanya Hossea na Kulunge kuwa wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) kwa kipindi cha miaka minne ijayo.