Samatta, Le Havre waanza na kipigo

NYOTA wa kimataifa wa Tanzania na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameanza vibaya Ligue 1 baada ya kikosi anachokitumikia kwa sasa Le Havre kulala kwa mabao 3-1 ikiwa ugenini mbele ya Monaco.

Samatta aliyesajiliwa hivi karibuni aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Simon Ebonog dakika ya 58, lakini haikuisaidia kuepuka kipigo hicho kwenye Uwanja wa Louis II mjini Monaco, Ufaransa.

Katika pambano hilo, Le Harve ilianza kwa kujifunga dakika ya 32 baada ya beki wa timu hiyo Gautier Lloris kutumbukiza  mpira wavuni katika harakati za kuokoa.

Kipindi cha pilia wenyeji ilipata mabao mengine mawili kupitia kwa

Eric Dier dakika ya 61 na Maghnes Akliouche dakika ya 74, huku bao la kufutia machozi la Harve  na Rassoul Ndiaye dakika ya 67.