Akizungumza leo (Agosti 19, 2025) katika hafla ya utiaji saini uliofanyika katika Ofisi za ADEM, Bagamoyo, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Innocent Mgeta, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, alisema mpango huo utahusisha mafunzo ya wakuu wa shule ana kwa ana na kupitia moduli za mtandaoni.
Amesema Mafunzo hayo yatahusisha kujenga uwezo wa wakuu wa shule za Sekondari yatakayoendeshwa kwa viongozi hao wa elimu ana kwa ana pamoja na mafunzo kupitia moduli za mtandaoni.
“Mbali na ushirikiano wa kitaasisi hizi, VVOB pia imefanya mashirikiano na Wizara ya Elimu kwa kipindi cha miaka sita ambapo inatarajiwa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023, ambayo inasisitiza matumizi ya Teknolojia”. Amesema
Kupitia ushirikiano huu, wakuu wa shule za Sekondari na maafisa elimu wa Halmashauri Idara ya Elimu Sekondari watapatiwa mafunzo kuhusu uongozi nausimamizi wa elimu utakaowawezesha kuboresha usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule za Sekondari nchini.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu – ADEM, Dkt. Maulid Maulid, amesema ushirikiano huo utasaidia serikali kufikia malengo yake kwa haraka kupitia mageuzi ya sera ya Elimu iliyoifanya.
Amesema kuwa taasisi yao inatarajia kunufaika kupitia ushirikiano huo katika masuala ya ujuzi wa TEHAMA na Amali ambapo itasaidia utekelezaji wa majukumu yao katika viwango vya kimataifa.
“Ushirikiano huu ni hatua ya kihistoria katika jitihada zetu za kitaifa za kuimarishauongozi wa shule. Kwa kuwajengea uwezo viongozi wa shule za sekondari kuhusuuongozi na usimamizi fanisi wa shule, tunajenga msingi wa kudumu wa kuboreshaufundishaji na ujifunzaji”.
“Tunajivunia kushirikiana na VVOB na wadau wenginekuhakikisha kila mwanafunzi nchini anapata maarifa katika Taasisi ya Elimu anayongozwa na viongozi wa shule walio na uwezo, weledi na maono.” Amesema Dkt. Maulid.
Nae Mkurugenzi wa Kimataifa wa Programu – VVOB, Tom Vandenbosch amesema ni tukio hilo ni mwanzo wa ushirikiano madhubuti na wenye matunda unaochagizwa namaono ya pamoja.
“Tunasikia Fahari na furaha kubwa kushirikiana na ADEM na tuna imani kwamba kwa pamoja, tutajenga mfumo thabiti na imara wa uongozi nausimamizi wa elimu, mfumo unaolenga ufanisi wa elimu kwa kila mwanafunzi.” Amesema
Amesema taasisi hiyo imelenga kuwajengea uwezo viongozi wa shule za sekondari nchini,ambapo utawasaidia kuendesha shule hizo vizuri kuendana na mabadiliko ya sera ya Elimu.
Vilevile Afisa Elimu (taaluma) Bagamoyo, Zaituni Shekovi amesema mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kutolewa kupitia mashirikiano ya taasisi hizo mbili ni muhimu kwani itasaidia katika usisimamizi wa walimu ili kuleta matokeo chanya ikiwemo ufaulu ili kuendana na mtaala mpya wa Elimu.
Ushirikiano huu unaratibiwa na Kituo cha Uongozi wa Shule Afrika (African Centre for School Leadership – ACSL).
