Mwanahabari mwandamizi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Sharon Sauwa amefariki dunia alfajiri ya kuamkia Jumanne Agosti 19, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baba mzazi wa Sharon, Steven Lamlembe amesema mazishi yatafanyika Agosti 21, 2025 katika makaburi ya Pugu Mwakenga nyuma ya Shule ya Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam.
Sharon, ambaye amekuwa MCL inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Ciziten, Mwanaspoti na Mwananchi Digital kituo chake cha kazi kilikuwa mkoani Dodoma.