Suluhu yazipeleka Sudan, Senegal robo fainali CHAN

SULUHU kati ya Sudan na Senegal imezivusha timu hizo kutinga robo fainali ya CHAN baada ya Congo kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Nigeria kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Sudan na Senegal zimetinga hatua hiyo baada ya zote kufikisha pointi tano tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo timu hizo za kundi D  zitakutana na washindi wawili wa kundi C katika robo fainali.

Hatua ya robo fainali inatarajiwa kuanza  Ijumaa kwa wenyeji Kenya kuvaana na Madagascar.

Timu zote mbili zilionyesha kuhitaji bao la kuongoza zilianza mchezo kwa kushambuliana kwa zamu huku safu za ulinzi zikionyesha uimara kutofanya makosa.

Kila timu ilifanikiwa kufika ndani ya 18 ya mpinzani wake, lakini uimara wa safu za ulinzi ulizifanya kuwa imara. 

Dakika mbili za mchezo zilisimama kupisha mwamuzi kuangalia VAR baada ya mchezaji wa Sudan kujiangusha ndani ya 18 katika dakika ya 44 ya mchezo ambapo uamuzi wa VAR ulithibitisha haikuwa penalti.

Hatd mwamuzi wa kati anapuliza filimbi kuashiria mapumziko hakuna timu iliyopata bao.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kuviziana dakika tano za mwanzo, laki hakukuwa na madhara kwa pande zote.

Sudan ilikuwa bora zaidi kutengeneza mashambulizi ikiliandama mara kwa mara lango la Senegal, lakini ilikosa umakini eneo la umaliziaji.

Ubora wa ukuta wa timu zote mbili umeufanya mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan kumalizika kwa suluhu.