…………..
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili jijini Dodoma kushiriki katika vikao vya kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa.
Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dkt.Mwinyi amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.