Kupitia kipindi cha Mapito cha Global TV, Shekhe Kandauma ameweka wazi msimamo wa Kiislamu kuhusu mambo yaliyo haramu, akisisitiza kuwa katu hayatawahi kubadilika.
Shekhe Kandauma alisema:
“Haramu itabaki kuwa haramu mpaka kiama.”
Ameeleza kuwa wanadamu hawana mamlaka ya kubadilisha mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu, na kwamba ni wajibu wa kila muumini kuzingatia mafunzo hayo kwa maisha ya dunia na akhera.
Akizungumza kwenye mahojiano hayo, Shekhe Kandauma alisema:
“Mama ni chuo kilichokamilika katika maisha yetu.”
Ameongeza kuwa thamani ya mwanamke ni kubwa duniani, akibainisha kuwa mchango wao ni msingi wa malezi, familia na jamii kwa ujumla.
Shekhe Kandauma alihimiza vijana na jamii kwa ujumla kuendelea kuwaheshimu na kuwathamini wanawake kama nguzo muhimu ya ustawi wa maisha.