Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, akiwataka wadau wa Uandaaji na usimamizi wa Bajeti kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa kutumia mafunzo waliyopata kuboresha utendaji, wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, akiagana na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha Bw. Raymond Kwohelera, baada ya kufunga mafunzo kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa kwa wadau wa Uandaaji na usimamizi wa Bajeti kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa yaliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine (kulia), akiteta jambo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa kwa wadau wa Uandaaji na usimamizi wa Bajeti kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa yaliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kikao kazi cha Wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, wakifuatilia maelekezo ya Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, wakati akifunga mafunzo kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS), yaliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, ukisikiliza hoja za wadau wa mafunzo ya Uandaaji na usimamizi wa Bajeti kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa yaliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada katika mafunzo kwa wadau wa Uandaaji na usimamizi wa Bajeti kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa yaliyofanyika kuhusu Mfumo Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mafunzo ya Mfumo Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya uandaaji wa mafunzo ya Mfumo Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, kwa wadau kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
…………………
Na. Peter Haule, WF, Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya amewataka Wataalam wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali kuzingatia mafunzo waliyoyapata ya kutumia Mfumo ulioboreshwa wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) katika kusimamia bajeti na kushauri namna bora ya kutekeleza bajeti zao.
Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma kwa niaba yake na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine wakati akifunga mafunzo ya Mfumo huo yaliyofanyika kwa siku tano.
Bw. Justine amewataka wadau waliopata mafunzo hayo kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na viongozi lakini pia kuyatumia mafunzo waliyoyapata kuleta mabadiliko chanya katika usimamizi wa bajeti katika maeneo yao.
Alisema kuwa mafunzo hayo yalilenga kuboresha utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali na kuongeza ufanisi katika mchakato wa bajeti na kuhakikisha vipaumbele vya Serikali vinatekelezwa ipasavyo, hivyo alieleza kuwa jambo hilo linatarajiwa kuonekana katika maeneo ambayo wadau hao wanayafanyia kazi.
Alisema mafunzo hayo yametolewa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza yalijikita katika mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa na awamu ya pili kwenye Tathmini ya Uandaaji wa Bajeti ya 2025/26 na tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya 2024/25.
Aidha amewapongeza wadau hao kwa kutoa maoni ambayo yatasaidia katika mchakato wa maandalizi ya Mwongozo wa uandaaji wa Mpango na Bajeti ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Aidha Kikao kazi cha awamu ya kwanza cha wataalamu wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, pamoja na mambo mengine, kimepata fursa ya kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/25.
Kikao kazi hicho pia kimejadili changamoto za uandaaji wa bajeti ya mwaka 2025/26 na kutoa maoni ya maandalizi ya Mwongozo wa uandaaji wa Mpango na Bajeti ya Serikali wa mwaka 2026/27 na kubaini maeneo ya kuboresha.