KATIKA mwendelezo wa kurejesha kwenye jamii, wakali wa ubashiri Meridianbet leo hii siku ya Ijumaa waliamua kuwafikia wakazi wa Kijitonyama Kisiwani kwaajili ya kutoa msaada wa mahitaji muhimu ya nyumbani.
Msafara huo wa kuwafikia wakazi hao uliongozwa na Mhariri mkuu wa kampuni hiyo Bi Nancy Ingram akiwa na jopo lake zima ambao kwa pamoja walifika na kupokelewa na wakazi wa eneo hilo kwani uhitaji ulikuwa mkubwa sana kutokana na wingi wa watu ambao uliopo hapo.
Msaada wa vyakula ambavyo vilitolewa ni pamoja na Mchele, sukari, unga wa ugali, unga wa ngano, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni etc. Msaada huo, uliowasilishwa leo unalenga kusaidia familia zenye uhitaji na kuleta tabasamu kwa wale ambao wanakumbwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula cha kutosha.
Hii sio mara ya kwanza kwa Meridianbet kurejesha kwenye jamii kwani mpaka sasa imekuwa ni desturi yao kuwajali wenye uhitaji kama tunavyojua jiji hili la Dar es salaam lina wingi wa watu hivyo kutokana na hilo uhitaji wa mahitaji ya nyumbani nao unakuwa ni mkubwa sana. Pia unaweza ukabashiri mechi za leo na wakali hawa wa ubashiri.
Mpunga upo kwenye michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Poker, Keno, Roulette, Aviator, Superheli hivyo ingia na ukusanye maokoto zaidi na zaidi. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz kubashiri mechi zote.
Safari hii ilikuwa ni zamu wa wakazi wa Kijitonyama Kisiwani kupata neema hii ambayo Meridianbet huitoa na pengine pia ni kwaajili ya kuwakumbusha na watu wengine pia wenye uwezo kuwakumbuka watu ambao wana uhitaji kwenye jamii zetu ambazo zinatuzunguka.
Wakizungumza wakati wa zoezi la kugawa msaada huo, wawakilishi wa Meridianbet walisema kuwa ni wajibu wa kila taasisi kushirikiana na jamii katika nyakati ngumu. “Tunaamini kuwa mafanikio ya kampuni yoyote hayawezi kutenganishwa na ustawi wa jamii inayotuzunguka. Ndio maana tumeona ni vyema kutoa mchango huu ili kupunguza makali ya maisha kwa ndugu zetu wa hapa Kisiwani,” alisema mmoja wa maafisa wa kampuni hiyo.
Baada ya kupokea msaada huo wa vyakula nao wakazi wa Kijitonyama, walisema kuwa “Huu msaada umetufariji sana. Tunaishukuru Meridianbet kwa kutukumbuka kwani si wengi wanaokumbuka jamii kama yetu,” alisema mama mmoja mkazi wa eneo hilo huku akibubujikwa na machozi ya furaha.
Msaada huu kutoka Meridianbet kwenda Kijitonyama Kisiwani ni zaidi ya msaada wa chakula ni somo la mshikamano, upendo na uwajibikaji kwa jamii. Ni mfano wa kuigwa na kampuni nyingine, na ni hatua moja mbele kuelekea Tanzania yenye mshikamano na maendeleo kwa wote.