Dk Asha Rose – Migiro katibu mkuu mpya CCM

Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemteua Dk Asha Rose-Migiro kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ni mgombea mwenza wa urais wa CCM.

Uteuzi wa Dk Migiro aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), umetangazwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla usiku wa leo Jumamosi, Agosti 23, 2025 makao makuu ya CCM, jijini Dodoma.

Makalla ametangaza hilo, saa chache tangu kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

Dk Migiro anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa kuwa mtendaji mkuu wa chama hicho tawala nchini Tanzania.

Endelea kufuatilia Mwananchi