Makalla awekwa kando CCM, Kihongosi amrithi

Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Kenan Kihongosi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafuzo wa chama hicho.

Kihongosi anachukua nafasi ya Amos Makalla ambaye ameachwa.

Uteuzi huo umefanyika leo Jumamosi, Agosti 23, 2025 katika kikao cha Halmashauri Kuu kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kihongosi amewahi kuwa mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa wa Simiyu kisha Arusha. Adha, amewahi kuwa katibu mkuu wa wa Umoja wa vijana na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.

Uteuzi wa Kihongosi umetangazwa usiku wa leo Jumamosi na Makalla wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CCM, jijini Dodoma.

Endelea kufuatilia Mwananchi