SINGIDA Black Stars imejiondoa katika dili la beki wa TMA, Vedastus Masinde baada ya kuanza mazungumzo na Mukrim Miranda wa Dodoma Jiji.
Iko hivi. Singida ilikuwa ya kwanza kumfuata Miranda, lakini baadae wakasitisha mazungumzo naye baada ya Pamba Jiji kuingilia dili hilo.
Inadaiwa pia Pamba Jiji imesitisha mazungumzo na Miranda na sasa Singida imemrudia tena ikimpelekea ofa nono na huenda akaibukia huko.
Hesabu za Singida zilikuwa kumtaka beki huyo wa Dodoma lakini baada ya kumkosa ilimfata Masinde kama mbadala wake na kwa kuwa wamefikia pazuri beki wa TMA wataachana naye.
“Singida walikuwa wanamhitaji Masinde kwa sababu Miranda alikuwa anatakiwa kwenda Pamba kwenda kule wamesitisha Pamba wamejitoa,” kilisema chanzo kutoka ndani na kuongeza:
“Baada ya Asinki kwenda Yanga wamejitoa kwenye dili la Masinde na kwa sasa wanamtazama Miranda kama mbadala wa beki huyo Mghana.”
Msimu mmoja alicheza timu tatu.