Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, Agosti 23, 2025 amemteua Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC) kuchukua nafasi ya Kenani Kihongosi.
Awali, Makalla alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nafasi ambayo Halmashauri Kuu ya CCM, imemteua Kihongosi kuishika.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Makalla ataapishwa Agosti 26, 2025, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma
Endelea kufuatilia Mwananchi