Rais Sri Lanka atupwa sero kwa matumizi mabaya ya fedha

Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) nchini Sri Lanka imemkata aliyekuwa Rais wa zamani wa Taifa hilo, Ranil Wickremesinghe kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali.

Wickremesinghe (76) amekamatwa baada ya kufika katika ofisi ya CID katika mji mkuu Colombo kutoa maelezo ya taarifa ya uchunguzi wa ziara yake ya London pamoja kuhudhuria sherehe ya kuhitimu kwa mke wake.

CID imedai kuwa kiongozi huyo alitumia fedha za Serikali kwa safari yake ya kibinafsi pamoja na walinzi wake jambo ambalo ni kinyume na sheria za taifa lao.

Jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha kukamatwa kwake kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha za umma.

Hata hivyo, Wickremesinghe amekanusha madai hayo na kueleza kwamba gharama za usafiri za mke wake zililipwa na yeye hakuna fedha za serikali zilizotumika. Kukamatwa kwake kunakuja siku chache baada ya CI na polisi kuwahoji wafanyakazi wake kuhusu gharama za usafiri huo.

(Imeandaliwa na Elidaima Mangela, kwa msaada wa mashirika)