KAMATI KUU CCM YAMPITISHA MASABURI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIVULE

:::::::

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kimempitisha mwanachama wa ambaye pia aliwahi kuwa Naibu instahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya ilala Ojambi Didas Masaburi kuwa Mgombea ubunge wa Jimbo la Kivule jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Masaburi ambaye aliongoza katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama hicho ametangazwa kuwa mgombea ubunge katika Jimbo hilo baada ya Kamati Kuu ya CCM kukaa kikao chake jijini Dodoma na kuchuja majina ya wagombea ubunge wake ambao watapeperusha bendera katika Uchaguzi huo.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amoss Makalla ametangaza majina ya wagombea ubunge katika majimbo yote ambapo katika jimbo la Kivule Mgombea ubunge aliyepitishwa na Chama hicho ni Ojambi Masaburi .

Baada ya kupitishwa kwa jina lake Masaburi atachukua fomu ya kugombea ubunge na kisha kuirejesha katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na hatimae kusubiria kampeni kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi katika Jimbo la Kivule.

Kwa kukumbusha tu Jimbo la Kivule ni Jimbo jipya ambalo limepatikana baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kuligawa Jimbo la Ukonga na kupatikana majimbo mawili ambayo Ukonga na Kivule na Jimbo hilo la Kivule Mgombea wake ni Masaburi.