Ni Sudan, Madagascar nusu fainali CHAN Kwa Mkwapa

BAADA ya kushindwa kupata mshindi ndani ya dakika 120, Sudan na Algeria zimelazimika kwenda katika changamoto ya mikwaju ya penalti ili kuamua mshindi wa mechi na hatimaye Sudan kuibuka kwa penalti 3-2.

Katika mchezo huo wa robo fainali ya CHAN uliopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar dakika 90 zimemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.

Sudan ilikuwa ya kwanza kupata bao katika kipindi cha pili baada ya makosa yaliyofanywa na beki wa Algeria na kusababisha Ayoub Ghelaza kujifunga dakika ya 48, lakini kupitia shambulizi kali Algeria ilisawazisha kwa bao la Soufiane Bayazid dakika ya 73.

Sudan ambayo msimu huu inashikiriki kwa mara ya nne CHAN, katika mashindano matatu iliyoshiriki awali ilimaliza nafasi ya tatu mara mbili ambapo mara ya kwanza 2011 ikiwa mwenyeji ilifika nusu fainali na kupoteza mbele ya Angola kisha ikacheza mechi ya mshindi wa tatu dhidi ya Algeria na kuibuka na ushindi wa mabao 1-0.

Ilishiriki mara ya pili 2018 na kumaliza mshindi wa tatu kwa kuichapa Libya kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2 na mwaka 2022 iliishia hatua ya makundi.

Kwa upande wa Algeria ambayo ndio ilikuwa mwenyeji wa mashindano yaliyopita kati ya  mara mbili ilizowahi kushirika moja  ilimaliza nafasi ya nne baada ya kuchapwa na Sudan 1-0 katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu. Pia katika mashindano iliyokuwa mwenyeji ilipoteza fainali mbele ya Senegal 2022 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 5-4.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Sudan kupata ushindi mbele ya Algeria baada ya  kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya miamba hiyo kwenye mechi mbili za mwisho zilizokutana katika michuano mbalimbali.

Baada ya kupenya Sudan takutana na Madagascar katika mchezo wa nusu fainali ambao utakapigwa Agosti 26 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.

2. Imeruhusu mabao mawili tu hadi sasa katika michuano hii ndani ya dakika 120.

3. Imecheza robo fainali ya nne na haijawahi kupoteza katika hatua hii. Ilishinda mbele ya Niger kupitia penalti 2011 na  kuitoa Zambia kwa bao  1-0 mwaka 2018 pamoja na leo dhidi ya Algeria.

4. Itaenda kucheza nusu fainali kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo 2011 na 2018.

5. Katika mechi za mtoano imeshinda mara nne na kufungwa mara tatu kati ya mechi saba.

6. Mechi pekee iliyoshindwa kufunga bao tangu ianze kushiriki michuano hii ilikuwa ni nusu fainali dhidi ya Nigeria 2018.

7. Imeshinda mechi yake ya pili kati ya saba zilizopita ilizocheza katika michuano yote.

1. Baada ya mechi ya leo inakuwa imetoka sare kwenye mechi nne zilizopita (ndani ya dakika 90) ndiyo rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi bila ushindi kwenye muda wa kawaida.

2. Hii inakuwa ni mechi yao ya kwanza kupoteza katika mechi  11 mfululizo.

3. Kichapo cha mwisho kwenye michuano hii kilikuwa dhidi ya Sudan kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu 2011 na leo imechapwa.

4. Haikuwa imeruhusu bao katika mechi nane kati ya 10  zilizopita.

5. Ilikuwa ni robo fainali yake ya tatu. Mbili zilizopita  ilishinda zote dhidi ya Afrika Kusini 2011 na dhidi ya Ivory Coast 2022.

6. Kabla ya mchezo huu, haikuwahi akupoteza robo fainali kwenye michuano hii, ilikuwa imeshinda zote na bila kuruhusu bao.

7. Hii ni mara ya kwanza Algeria kutolewa mapena kwenye michuano ya CHAN katika mara zote ilizoshiriki.

8. Katika mechi saba za mtoano ilizocheza kwenye michuano hii imeshinda tatu na kufungwa nne.

9. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Algeria kufika hadi hatua ya changamoto ya mikwaju ya penalti katika mechi ya mtoano ya michuano ya CHAN, mara zote ilikuwa ikimaliza ndani ya dakika 90.