ANGELA KAIRUKI ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KIBAMBA KUPITIA CCM


 Pazia la uchukuaji wa fomu za kuwania ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limefunguliwa rasmi leo, ambapo mwanasiasa mahiri Angela Kairuki amechukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Kibamba.

Fomu hiyo imekabidhiwa kwake na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Ubungo, Bi. Rose Mpeleta. Mara baada ya kukabidhiwa fomu, Kairuki alieleza kuwa yeye na timu yake wako tayari kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kibamba kwa moyo wa dhati.

Aidha, ameahidi kufanya kampeni za kistaarabu, zenye kuheshimu misingi ya demokrasia na mshikamano wa kitaifa, akisisitiza kuwa lengo lake ni kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kibamba endapo atapata ridhaa ya kuwatumikia kama Mbunge wao.