Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akimpongeza Meneja wa Barrick nchini Dk. Melkiory Ngido (kushoto) kwa udhamini wa CEOs Forum 2025 kulia kwake aliyeshika cheti ni Mwenyekiti wa Bodi ya Twiga, Casmir Kyuki.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya Twiga, bw. Casmir Kyuki (kulia) baada ya kumkabidhi cheti cha udhamini (kushoto) ni Meneja wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido.
Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido akiongea katika CEOs Forum kuhusu mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Serikali
Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido akiongea katika CEOs Forum kuhusu mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Serikali
Baadhi ya washiriki na wadhamini katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko.
*
Kampuni ya Barrick yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imetunukiwa cheti cha tuzo kwa kudhamini kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichomalizika leo jijini Arusha.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt. Doto Biteko ambaye alikuwa mgeni rasmi wa kufunga kikao hicho cha siku nne ambapo pia alitoa tuzo kwa taasisi nyingine zilizodhamini mkutano huo.
Akiongea kuhusu udhamini huo kabla ya kukabidhiwa cheti cha tuzo,Meneja wa Barrick nchini Dkt. Melkiory Ngido amesema kampuni imedhamini kikao hicho kama mdau mkubwa wa maendeleo inayoamini kuwa sekta binafsi na Serikali zikishirikiana zinaweza kuleta matokeo Chanya kwenye uchumi wa nchi kama inavyoonyesha kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025-2050.
Dkt. Ngido pia amesema Barrick imekuwa ikitekeleza falsafa ya 4R ya Rais Samia kwa vitendo ambayo imeleta ufanisi katika uendeshaji wa shughuli zake nchini kwa kushirikiana na Serikali ambapo imekuwa kioo cha uwekezaji wenye mafanikio nchini.
“Kupitia uwekezaji wetu na uendeshaji wa shughuli zetu kwa ubia na Serikali tumepata mafanikio makubwa baadhi yake yakiwa ni kuwa kinara wa kulipa kodi na tozo mbalimbali ,kutoa gawio nono kwa Serikali,kunufaisha wazabuni wa ndani na kupanua wigo wa ajira kwa watanzania, matumizi ya teknolojia za kisasa na kufanikisha miradi mikubwa ya kijamii hususani katika sekta za elimu,afya,miundombinu kupitia fedha za CSR zinazotolewa na migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara”.
Dkt. Ngido amesema kuwa kampuni inaendelea kufanya tafiti mbalimbali za kijiolojia kwa lengo la utambuzi wa maeneo mapya ya uchimbaji na imeweza kurefusha maisha ya migodi yake kwa muda mrefu zaidi na kuendelea kunufaisha taifa.