Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika mapema Leo, jijini Dar-es-Salaam, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji,Mh.Prof.Kitila Mkumbo, amesema anawashukuru na kuwapongeza Kampuni hiyo ya Vodacom kwa kuandaa mdaharo mzuri wa kuandaa Watanzania katika Utekelezaji wa Dira 2050, ambao utaanza rasmi tarehe, 1 Julai,2026.

Amesema mjadala huo ulikuwa mzuri kuhusu utekelezaji wa Dira 2050, ikilenga sana ni namna gani kila Mtanzania atakuwa na fursa ya kutumia teknolojia za Kidigitali na apate kuwa na fursa ya kutumia nyenzo hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yeye mwenyewe lakini pia kushiriki maendeleo ya Nchi.
“Na Sisi kama Serikali tumeandaa Mazingira mazuri ili wawekezaji waweze kuwekeza na kuna ambao wameshaanza kuja kuweka Viwanda vya kuzalisha vifaa vya digitali ikiwemo simu lakini pia Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ikiwemo kupunguza kodi katika vifaa hivi, ili Watanzania waweze kununua simu janja kwa sababu ni nyenzo za muhimu sana za maendeleo za kutafuta ajira n.k.
“Tumeona Vodacom Wana dirisha maalum la Vijana kwa ajili ya vijana karibu milioni Tano,wanalitumia hivyo sisi tumekuja na nyenzo mbalimbali kwa mfano tumeanzisha mfuko maalum wa kuweza kuwasaidia vijana kupitia biashara mpya waweze kupata mitaji ya kuweza kujishughulisha hususani wale wanaotumia Kidigitali,” amesema Prof.Mkumbo.
Nae Mkuu wa Uhusiano na Vyombo vya Habari Vodacom Tanzania,Annette Kanora amesema kuwa, wamezindua Ripoti yao ya mwaka ya ESG ambayo inaangalia jinsi mkakati wao ambao wametimiza kwa Mwaka wa fedha uliopita na umeisha Machi,31, 2025 na hasa ni kuangalia ni jitihada gani ambazo wamezifanya katika maeneo makuu matatu ambayo ni kuwezesha watu,kutunza Mazingira,na kudumisha uaminifu na wadau wao mbalimbali.