Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekabidhiwa rasmi Ofisi ya Mjumbe Maalum wa Masuala ya Wanawake Amani na Usalama Barani Afrika, aliyoteuliwa mwaka huu.
Balozi Mulamula amekabidhiwa ofisi hiyo leo, jijini Addis Ababa, Ethiopia na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, (AUC), Mahmoud Ali Youssouf, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibout.
Balozi Mulamula aliteuliwa katika nafasi hiyo, mwaka huu akichaguliwa na viongozi mbalimbali wanaounda Umoja wa Afrika kutokana na uzoefu wake mkubwa alionao katika uongozi wa siasa za kimataifa, akishiriki katika mikutano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo kufanya usuluhishi wa migogoro mbalimbali ya kimataifa.
Akikabidhiwa ofisi hiyo kuanza rasmi kazi, Nchini Ethiopia, Balozi Mulamula aliwashukuru viongozi wa Afrika kwa kumwamini na kumteua katika nafasi hiyo huku akiahidi kazi kubwa katika kuwawakilisha wanawake wa Afrika na kutetea maslai yao.
Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Viongozi Wanawake (WPL), Neema Lugangira, alimpongeza na kumtakia heri katika majukumu yake hayo mapya.