MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Kisutu, Tousif Bhojani, amewataka wananchi wa kata hiyo kumpa kura za kishindo mgombea urais kwa kitekiti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa Okotoba 29 mwaka huu.
Ameyasema hayo Dar es Salaam, leo baada ya kurejesha fomu ya uteuzi wa udiwani katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kata hiyo, wilayani Ilala.
Bhojani ambaye alipita katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo kupongezana na wananchi, amesema ikiwa atateuliwa na wananchi kumchagua atahakikisha Kisutu inapiga hatua kubwa kimaendeleo na kwamba hakuna atakayeachwa katika maendeleo hayo.
“Mpeni kura nyingi za kishindo mgombea wetu wa urais kwa tiketi ya CCM Rais Dk. Samia. Oktoba twende kwa wingi tukatiki. Nichagueni mimi niwaletee Kisutu mpya. Kisutu ya maendeleo na Kisutu yenye mabadiliko,”ameeleza mgombea huyo.