RAIS MSTAAFU KIKWETE:WANAOSEMA UTARATIBU HAUKUFUATWA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM WANAJITOA UFAHAMU

Asema utaratibu uliotumika kumpata Dk.Samia kuwa mgombea Urais ndio huo huo uliotumika kwa wengine huko nyuma

*Asema wanaosema utaratibu umekiukwa walikuwepo awamu zote lakini kwanini wanasema hayo leo

*Asisitiza utaratibu wa Mkutano Mkuu uliofanyika Januari 18 na 19 uko sahihi na anauunga mkono 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, amewajibu wale wote ambao wamekuwa waliopitishwa umma wa Watanzania kwa makusudi eti utaratibu wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Samia Suluhu Hassan ambapo amesema watu hao ni wazushi na wameamua kujifanya hamnazo.

Kikwete amesema kwamba CCM imekuwa na utaratibu wa kupata wagombea wake Urais tangu kuanza kwa Mfumo wa Vyama vingi nchini na utaratibu wa kumpata Dk.Samia kuwa mgombea ndio utaratibu ambao umetumika kupata viongozi wengine waliongoza nchi yetu ya Tanzania katika awamu zote zilizopita kuanzia awamu ya pili.

Ameyasema hayo leo Agosti 28,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani katika Uwanja Tanganyika Packers wakati wa uzinduzi rasmi za kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi.

Akieleza zaidi Rais Mstaafu Kikwete ametumia nafasi hiyo kufafanua hatua kwa hatua kuhusu mchakato uliotumika kumpata Dk.Samia kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 ambapo amesema wanaosema utaratibu haukufuatwa huenda hawafahamu utaratibu wa chama au pengine wanajitoa ufahamu kwa kujifanya hamnazo.

Kikwete aliyekuwa akieleza kwa utaratibu kuhusu mchakato huo ameeleza tangu kuanza kwa mfumo wa Vyama vingi nchini ndani ya Chama chao cha CCM wamekuwa na utaratibu Rais aliyekuwa madarakani kupewa nafasi ya kukamilisha awamu ya pili ya uongozi baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya uongozi wake.

Ameongeza kuwa utaratibu huo wa kumpata mgombea Urais ambao umetumika kwa Dk.Samia ambapo Mkutano Mkuu ulipitisha jina lake ndio Mfumo ambao umetumika tangu zamani akitoa mfano tangu enzi za kumpata Rais Mstaafu Benjamin Mkapa,yeye(Jakaya Kikwete) Rais Hayati Dk.John Magufuli na ndio huo huo umetumika kwa Dk.Magufuli.

Amesisitiza kwamba hivyo ndio imekuwa is ikifanyika hivyo amehoji kwanini wanaotoa kauli za kuzua taharuki katika awamu hii inayoongozwa na Rais DK.Samia.”Sasa kumekuwa na kekele nyingi na kwanini kelele hizo ziwe sasa na ionekane tofauti kwa Samia.

“Watu wanaosema maneno hayo walikuwepo tangu enzi za Mkapa, mpaka sasa na huko kote walikuwa kimya hawakusema lolote lakini kwanini iwe sasa watu hao hao wanakuja na maneno ya kupotosha utaratibu ule ule kwa Dk.Samia.”

Wakati akiendelea kueleza kuhusu utaratibu huo wa kumpata Dk.Samia kuwa mgombea Urais wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu Kikwete amesema kwamba baada ya mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Januari mwaka huu kutoa azimio la kumpitisha Dk.Samia kumekuwa na maneno mengine na wapo ambao wanamsema yeye kwa kuwa alikuwepo katika mkutano ule .

Kuhusu sababu za wana CCM kusema Rais Samia mitano tena inatokana na kazi kubwa na nzuri ambayo ameifanya katika uongozi wake na hoja ya mitano tena iliibuka katika mkutano Mkuu wa Chama hicho na hiyo inatokana na sababu za kutekeleza vema Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya 2020-2025 sambamba na utekelezaji wa miradi mikubwa iliyokuwa inahitaji fedha nyingi ambayo iliachwa na mtangulizi wake.

Aidha amesema kuwa Dk. Samia alipokea nchi katika kipindi kigumu baada ya kufariki dunia aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli na kuongeza l hofu ilitanda kama ataweza kutekeleza miradi hiyo au laa.”Chini ya Rais Samia ameuthibitishia umma ameyaweza mamlaka ya Urais na Amiri Jeshi Mkuu.

Kikwete amesema kuwa nchi imeendelea kuwa yenye amani, umoja, mshikamano na maendeleo yanaonekana na kufafanua kuwa Dk.Samia hakuwa na muda wa kuunda timu yake na sera zake ukilinganisha na watangulizi wake lakini katika muda mfupi baada ya kukaa madarakani amethibitisha kuwa uongozi na anauwezo na ndio maana leo wamekutana tena kuwapmba Watanzania kumchagua tena kuongoza nchi yetu.