
Dkt.Kikwete Aweka Wazi: Uteuzi wa Samia Ulifuata Taratibu, Wasioelewa Wana Upungufu wa Maarifa
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameweka bayana kuwa mchakato wa kumpitisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, umefuata utaratibu uleule wa siku zote unaotumika ndani ya chama hicho tangu enzi na enzi. Akihutubia…