…………
Chama cha siasa cha Kijamii CCK kimesema moja ya kipaumbele chake katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu kitaweka mikakati mizuri kwa vijana ikiwemo kuboresha elimu imara itakayomsaidia mtanzania kuweza kujiajiri.
Mwenyekiti wa Chama hicho na Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania David Mwaijojele amesema hayo leo wakati akizungumza jijini Dar es salaam akielezea kampeni ya chama hicho ambayo watakwenda kuizindua siku ya kesho Agosti 30 katika kata ya Kijichi Wilaya ya Temeke.
Amewasisitiza malengo yao ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na furaha ya kuishi maisha bora na kumtoa katika hali ya umaskini na sio kuwa na matabaka.
“Tuna vipaumbele vizuri kikiwemo kwa ajili ya ajira hivyo CCK tumejipanga kuhakisha tunaweka mazingira mazuri katika sekta mbalimbali ili wananchi wetu waweze kunufaika napo”amesema Mwaijojele
Aidha Mgombea huyo amesema wameingia kwenye uwanja wa kunadi sera zao kwa kuelezea vipaumbele vyao kwa ajili ya kumkomboa mtanzania kutoka kwenye maelezo ya kwenye vitabu na makaratasi.