CHUO CHA FURAHIKA CHAWEKA MIKAKATI KUWAKOMBOA VIJANA 300 KWA KUWAPATIA MAFUNZO

NA VICTOR MASANGU

Katika kuunga mkono juhudi mbali mbali zinazofanywa na  Rais wa  awamu ya sita. Dkt. Samia Suluhu Hassan hususan katika kundi la vijana uongozi wa chuo cha Furahika education College (FEC) kilichopo Jijini Dar es Salaam inatarajia kuwapatia  mafunzo ya fani mbali mbali kwa vijana wapatao 300 ambapo watapataa fursa ya kusoma masomo tifauti kwa kipindi cha mwaka mmoja bure bila malipo yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu mkuu wa chuo hicho cha  Furahika Dkt. David Msuya amesema kwamba lengo kubwa  la mafunzo  hayo ni kwa aajili ya kuweza  kuwasaidiaa vijana kuondokana na wimbi la matumizi yaa madawa ya kulevya ikiwa pamoja na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika maakundi mabaya.

Msuya amebaainisha kwamba  chuo chao  kimeamua  kushirikian bega kwa bega na serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia,  wanawake na makundi maalum  katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa mafunzo hayo bure kwa lengo la kuwasaidi vijana kupat ujuzi n maharifa mbali mbali bila malipo yoyote.

“Chuo chetu cha Fuhahika kwa sasa tumeamu kuung mkono juhudi za serikali y wamu y sit n kwamba tunshirikiana na Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia, wanawake na makundi maalum na hii yote ni kwa ajili  ya kuwasaidia vijana wetu kupata mafunzo na ujuzi wa fani mbali mbali  ili wasiweze  kujingize katika makundi mabaya ikiwemo kujihusisha na madawa ya kulevyaa pamoja ngono,”amebaainish Dkt Msuya.

Kaimu mkurugenzi huyo amebainisha kwamba vijana hao  300 aambaao wanatarajia  kuanza rasmi mafunzo hayo mwezi 0ctoba mwaka huu  na kubainisha kwamba  zoezzi la usahili kwa wanafunzi  hao unatarajiwa  kuanza kufanyika  tarehe 2 mwezi wa tisa kupitia tovuti ya chuo au kwenda  katika ofisi zao zilizopo maeneo ya  Buguruni malapa.

Aidha Msuya amezitaaja badhi ya kozi ambazo watafundishwa vijana hao ni pamoja na ufundi selemala,mapishi,kompyuta (ICT) ,upigaji wa picha,masuala ya bandari,kozi na ususi,kozi ya udereva, biashara  na masoko, kozi ya utalii pamoja na fani nyingine mbali mbali za uongozi katika mambo ya kibiashara.

“Pia amewahimiza wazazi, walezi pamoja viongozi wa chama wakiwemo wale wa jumuiya kuhaakikisha wanawahimiza vijanaa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kupta ujuzi mbali mbali naa hatimaye kuweza kujiajiri na kuondokana na kuwa tegemezi,”amebinisha Msuya.

Katika hatua nyingine Msuya amebainisha kwamba watapatiwa mafunzo hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo gharama zake zote zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zimetolewa  na wafadhili kutoka nchini Ujerumani kwa lengo la kuweza kuwakomboa vijana kutoka Tanzania bara na visiwani ambao wameshindwa kujiendeleza na wengine hawana ujuzi wowote.