DKT. NCHIMBI ATIA MGUU MWANZA KUOMBA KURA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

::::::::

Na Mwandishi Wetu,Mwanza 

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi  amewasili Mkoa wa Mwanza Leo Agosti 29, 2025 kwa ajili ya Kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

 Balozi Dkt Nchimbi anatarajia kufanya mikutano mbalimbali kwa ajili ya kuzinadi sera pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya 2025-2030.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingia siku ya pili za kampeni zake baada ya jana kuzinduliwa rasmi hapo jana jijini Dar es Salaam  na Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan 





Mwisho