BALOZI DKT. NCHIMBI ATEMBELEA NYUMBANI KWA BABA WA TAIFA

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kijijini Mwitongo,Butiama na kuzuru kaburi la mwasisi huyo wa Tanzania na CCM.

Dkt.Nchimbi ameingia mkoani Mara hii leo Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya watanzania katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.