Morocco yatwaa ubingwa wa CHAN 2024

Timu ya taifa ya Morocco, ‘Simba wa Milima ya Atlas’ imetwaa ubingwa wa Fainali za CHAN 2024 baada ya kuifunga Madagascar kwa mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani, Kenya.

Hili linakuwa taji la tatu kwa Morocco linaloifanya iwe timu iliyotwaa mara nyingi ubingwa wa CHAN,  ambapo awali ililibeba mara mbili mfululizo 2018 na 2020.

Kwa kutwaa ubingwa huo Morocco itapata zaidi ya Sh 8.77 bilioni huku mshindi wa pili Madagascar ikijihakikishia kupata zaidi ya Sh 3 bilioni.

⚽️ 09″ Felicite                           

⚽️ 68″ Toky