…………..
Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Dkt. Lameck Karanga amesema Serikali kupitia mamlaka husika imeanza kuchukua hatua dhidi ya raia wa kigeni pamoja na waongoza watalii ambao ni watanzania wanaotuhumiwa kuwarekodi maudhui yasiyofaa wananchi wa kabila la Wahadzabe wanaoshi wilayani humo.
Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 Agosti 27,2025, Dkt. Lameck ameeleza kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji baada ya kuwakamata na kuwahoji raia hao wa kigeni wamebaini kuwa hawaishi kihalali nchini kutokaka na vibali vyao kuisha muda wake huku akieleza kuwa hatua stahiki dhidi yao zitachukuliwa.
Aidha, ameeleza kuwa waongoza watalii walioshiriki katika tukio hilo la kabila hilo, wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufungiwa kupeleka watalii katika eneo la Wahadzabe lenye urithi adhimu na adimu wa kiutamaduni.