Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Gairo
MAMIA ya wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan na kauli yao ni moja tu Oktoba wanatiki kwake.
Akiwa katika mkutano huo wa kampeni leo Agosti 30,2025 wilayani Gairo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesema Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020-2025 imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 95 na sasa wanaomba tena ridhaa ya wananchi ili kuendelea kuwatumikia kwa miaka mingine ijayo 2025-2030.
Amesema kuwa CCM ni Chama ambacho hakina rongorongo kinachoahidi kwa wwnanchi kinatekeleza na hiyo imefanya Chama kuendelea kuaminiwa.
Kwa wananchi hao wa Wilaya ya Gairo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameelezea hatua ambazo zinachukuliwq katika kuboresha huduma mbalimbali huku akitoa ahadi ambazo zitatekelezwa kwa miaka mingine mitano ijayo iwapo Oktoba 29 mwaka huu atachagulia .
“Katika kipindi cha pili cha miaka mitano tunakwenda kushughulikia barabara ya Lubeho -Kiswiti lakini Tabu Hoteli -Kitange ,Chakwale-Mtumbatu,na Chakwale – Lesaka.Pia barabara nyingine ni Gairo -Nongwe ambayo itakamilshwa .
“Barabara hizo zinakwenda kuwa na lami lakini ahadi nyingine tunakuja kuongeza vituo vya afya vingine vitano katika kata za Rubeho ,kata ya Idigo,Chakwale, Madenge na Leshata pamoja Zahanati 10 zinakuja kwenye Jimbo hili.Pia tutajenga Machinjio manne ndani ya Wilaya ya Gairo
Ahadi nyingine ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Wilaya ya Gairo ni kwamba Serikali itakamilisha Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Gairo ili vijana wakasome wapate ujuzi wajiairi.