::::::::
Jiji la Dar es Salaam lililipuka kwa shangwe katika viwanja vya Tanganyika Packers – Kawe wakati wa uzinduzi wa Chrome, chapa mpya kutoka Serengeti Breweries Limited (SBL). Ikiwa na ladha mbili – Gin na Vodka – Chrome imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya ma-hustler wa Tanzania: vijana wanaopambana kila siku, wanaoamini kuwa siku moja watafanikiwa, na kusherehekea ushindi wao – iwe mdogo au mkubwa – pamoja na marafiki, familia na wale waliowasaidia kufika walipo leo.
Kutoka Kariakoo mpaka Kinondoni, na kutoka mitaa mbalimbali ya Dar, ma-hustler walikusanyika kwenye mji wa Chrome City kusherehekea safari na mafanikio yao.
“Chrome sio tu kinywaji. Ni chapa inayosimulia hadithi ya hustle, ustahimilivu na mafanikio ya vijana wa Kitanzania. Yawe mafanikio madogo au makubwa, Chrome ipo kusherehekea kila hatua ya safari hiyo,” alisema Gwamaka Mwankusye, Meneja wa Habari wa Serengeti Breweries Limited.
Uzinduzi huu haukuhusisha tu muziki na burudani, bali pia uliwapa nafasi wajasiriamali kuonesha hustle zao na kukutana na wateja wapya. Mbunifu wa mitindo, Audrey Erasrus, alisema: “Jukwaa hili limekuwa msaada mkubwa kwetu wabunifu. Nimekutana na watu wanaoweza kuwa wateja wangu wa muda mrefu na limekuwa fursa ya kutambulisha kazi zangu kwa hadhira kubwa zaidi.”
Msanii wa tattoo, Simba Lameck, naye aliongeza: “Kwa kazi zetu, exposure ndiyo kila kitu. Uzinduzi huu ulinipa nafasi ya kuonesha ubunifu wangu na kupata wateja wapya mara moja. Ni hatua kubwa kwa hustle yangu.”
Kadri usiku ulivyokuwa unaendelea, nguvu na shangwe viliongezeka zaidi kupitia burudani za aina yake kutoka kwa DJ maarufu nchini Mister Joozey pamoja na wasanii wanaong’ara kwa sasa D Voice na Dogo Rema. Umati ulifurahia na kucheza huku wakiburudika na Chrome, wakienzi moyo wa upambanaji wa hustler halisi wa Dar.
Kupitia uzinduzi huu, Chrome imedhihirisha kwamba – sio kinywaji pekee, bali ni mtindo wa maisha uliojengwa mahsusi kuenzi hustle, uthubutu na mafanikio ya vijana wa Kitanzania – roho halisi ya jiji la Dar es Salaam na kwingineko zaidi.
Mwisho