:::::::::
Dar es Salaam ilishuhudia usiku wa burudani na sherehe zisizosahaulika pale Tanganyika Packers – Kawe, wakati wa uzinduzi wa Chrome Gin, kinywaji kipya kinacholenga kusherehekea hustlers wa Tanzania.
Kwa mara ya kwanza, hustlers kutoka maeneo mbalimbali ya jiji waliunganishwa pamoja – kuanzia Manzese, Kariakoo hadi Kinondoni – wote wakija kusherehekea ushindi wao, mdogo au mkubwa, wa kila siku.
“Chrome Gin imewaleta hustlers pamoja kusherehekea ushindi wao – iwe ni kufanikisha dili kubwa au kufanikisha hustle ya kila siku. Hii ndiyo hamasa ambayo tunapenda kuisambaza kwa vijana wote wanaopambana nchini ili kufikia malengo yao na sababu ya Chrome Gin kuwepo,” alisema Gwamaka Mwankusye, Meneja wa Habari wa Serengeti Breweries Limited.
Lakini haikuwa tu kuhusu burudani; tukio hili pia liliwapa nafasi wajasiriamali wadogo na wakubwa kukutana na wateja wao pamoja na kujitangaza sokoni. Audrey Erasrus, mbunifu wa mavazi, alieleza: “Tukio hili limekuwa jukwaa kubwa kwetu wabunifu. Nimekutana na watu wapya ambao wanaweza kuwa wateja wangu wa kudumu na pia kuongeza jina langu mitaani.”
Simba Lameck, msanii wa tatoo, naye hakuachwa nyuma: “Kama msanii wa tatoo, mara nyingi tunategemea maneno ya mdomo kufika kwa watu. Hii event imenisaidia kujitangaza kwa hadhira kubwa na kukutana na wateja wapya ambao tayari wameonyesha nia.”
Kama haitoshi, usiku uliwaka moto kwa burudani kali kutoka kwa DJ Joozey, D Voice na Dogo Rema, ambao waliitikisa stage kwa nguvu, huku hustlers wakiburudika, wakicheza, na kufurahia ladha ya kipekee ya Chrome Gin.
Uzinduzi huu wa Chrome Gin umethibitisha kitu kimoja muhimu: hustlers wa Dar wanaposherehekea, wanafanya hivyo kwa style, kwa muziki, na kwa kinywaji kipya kinachoelezea ushindi wao – Chrome Gin.
Mwisho.