Mchezaji Jesus Ducapel Moloko aliyewahi kukipiga kunako klabu ya Yanga SC na AS Vita Club, amejiunga na AS Kigali kwa mwaka mmoja, msimu wa 2025/26.
AS Kigali ni miongoni mwa timu zinazojiandaa na msimu ujao, hasa michuano ya Ligi ya Rwanda, itakayoanza mechi zake Septemba 14, 2025, dhidi ya Amagaju FC.
AS Kigali imemsajili Jesus Ducapel Moloko kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwakosa wachezaji iliokuwa inataka kuwasajili.
Moloko (27), amecheza katika klabu mbalimbali, kama AS Vita Club ya DRC mwaka 2021, Yanga SC ya Tanzania, Al Sadaqa na Diyala ya Iraq, kabla ya kujiunga na ES Mostaganem ya Algeria.
Related