Morocco Mabingwa wa Afrika Mashariki CHAN 2024 – Global Publishers


HATIMAYE Pamoja CHAN 2024 imegota mwisho na mabingwa wakiwa ni Morocco baada ya kuoata ushindi katika mchezo wa fainali, Agosti 30 2025.

Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Moi, Nairobi umesoma Madagascar 2-3 Morocco.
Katika mchezo wa leo mabao ya Madagascar yamefungwa na Felly dakika ya 9 na bao la pili limefungwa na Toky Rakotondraibe dakika ya 69. Kwa upande wa Morocco ni Youssef Mehri dakika ya 27, Oussama Lamlioui dakika ya 44 na 80.

Oussama ni mfungaji bora wa Pamoja CHAN 2024 akiwa ametupia jumla ya mabao 6 huku Mohamed Hrimant wa Morocco akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.

Mshindi wa tatu ni Senegal ambaye alipata ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Sudan katika mchezo uliochezwa Agosti 29 2025 Uwanja wa Mandela, Kampala Uganda baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Tanzania iliishia hatua ya robo fainali katika CHAN 2024 ilifungashiwa virago na Morocco iliyokuwa Kundi A na Kenya ambayo iliongoza kundi.

Ikumbukwe kwamba Morocco kwenye hatua ya makundi ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Kenya ikamaliza ikiwa nafasi ya pili. Tanzania kwenye hatua ya makundi ilipata ushindi dhidi ya Madagascar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Timu za ukanda wa CECAFA zimegotea hatua ya robo fainali asilimia kubwa huku Sudan ikifurukuta mpaka mshindi wa nne katika CHAN 2024.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.