SIKU tatu tu tangu kikosi cha timu ya taifa ya Uganda The Cranes kutangwazwa huku majina ya nyota wa zamani wa Yanga, Khalid Aucho na mshambuliaji wa Simba, Steven Mukwala kutojumuishwa upepo umebadilika kwa wachezaji hao.
Taarifa kutoka Uganda zinasema kuwa, nyota hao wameongezwa katika kikosdi hicho kinachojiandaa na mechi mbili za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za 2026, baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka wa nchini humo.
Koch Paul Put hakuwajumuisha nyotai hao katika kikosi cha awali cha wachezaji 28, lakini jana Shirikisho la Soka la Uganda (FIFA) liliwatangazwa kuwaita ghafla ya kutakiwa haraka kujiunga na timu hiyo inayojiandaa na mechi mbili za Kundi G dhidi ya Msumbiji na Somalia zitakazopigwa kati ya Septemba 5 na 8 mtawalia.
Aucho ndiye nahodha wa kikosi hicho na taarifa za Fufa zimemtaka yeye na Mukwala kujiunga na timu kesho Jumatatu tayari kwa kambi ya maandalizi ya mechi hizo za kuwania fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani katika nchi ya Marekani, Canada na Mexico.
“Kikosi cha Uganda The Cranes kitaanza kukusanyika Agosti 31 (leo) Jumapili katika hoteli ya FUFA Kisaasi kikiongozwa na wachezaji 11 na CHAN. Waliongezwa karibuni ni nahodha Khaluid Aucho na Steven Mukwala ambao wanategemewa kujiunga na timu Jumatatu ya Septemba Mosi na kufanya idadui ya wachezaji wote kuwa 30,” ilifafanua taarifa hiyo ya Fufa.
Uganda itaanza kuvaana na Msumbiji Septemba 5 kabla ya kumalizana na Somalia Septemba 8 na wachezaji walioitwa awali kabla ya Aucho na Mukwala kuongezwa ni pamoja na; Denis Onyango, Salim Magoola, Nafia Aliozi, Joel Mutakubwa, Elvis Bwomono na Herbert Bockhorn.
Wengine ni Elio Capradossi, Rogers Torach, Toby Sibibick, Hilary Mukundane, Joradan Obita, Aziz Kayondo, Herbert Achayi, Gavin Kizito, Ronald Ssekiganda, Kenneth Semakula, Joel Sserunjogi, Abdulkarim Watambala, Travis Mutyaba na Denios Omedi.
Pia wamo Allan Okello, Joseph Mpande, Rogers Mato, Reagan Mpande, Juse Ssemugabi, John Dembe, Patrick Kakande na Ochechukwu Ikpeazu.