Sita wakamatwa tuhuma za rushwa, mgombea ubunge atimka

Tabora. Watu sita wanashikiliwa na vyombo vya usalama Mkoa wa Tabora wakidaiwa kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa wagombea ubunge wa Nzega Mjini mkoani humo, huku wengine 40 wakisakwa akiwemo mgombea husika. Mgombea huyo wa ubunge ambaye jina limehifadhiwa amekimbia na kutelekeza gari katika Mtaa wa Musoma wilayani Nzega Mkoa wa Tabora ambapo ukaguzi uliofanywa…

Read More

MKAKATI ENDELEVU WA KAMPUNI YA BARRICK WAFANIKISHA KULETA MABADILIKO CHANYA KWENYE JAMII KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 6

  Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mining Corporation Mark Bristow – Picha kutoka Maktaba Toronto- Kampuni ya Madini ya Barrick (NYSE:B)(TSX:ABX) imefanya mkutano wa mwaka kutoa mrejesho wa mkakati wake endelevu,unaojumuisha ushirikiano wake na wadau ukijikita kuhusu utekelezaji wa mkakati endelevu na vipaumbele.Mkutano huo wa kimtandao unafuatia ripoti ya kina ya Mkakati Endelevu ya…

Read More

Rostam Aziz: Mchakato mpya wa CCM ni wa haki zaidi

Dar es Salaam. Kada nguli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz amepongeza mchakato mpya wa chama hicho katika kupitisha wagombea wa ubunge akisema unatoa nafasi ya haki na uwazi kwa watiania. Akizungumza leo, Jumapili Agosti 3, 2025 jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu, Rostam amesema amewahi kupitia michakato mingi ya…

Read More

Uchumi wa buluu unavyoinua uchumi ukilinda mazingira

Tanzania imeanza kuchukua hatua madhubuti kuelekea mageuzi ya kiuchumi kwa kuwekeza katika uchumi wa buluu, ikiwa ni sehemu ya mpango wa muda mrefu ulioainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Dira hiyo inatambua sekta ya uchumi wa buluu kama moja ya nguzo muhimu za kimageuzi zinazoweza kuongeza kasi ya maendeleo endelevu, kupunguza umaskini na…

Read More

Vita katika sanduku la kura CCM, majimbo haya hapatoshi

Dar es Salaam. Kinyang’anyiro cha kuisaka tiketi ya kugombea ubunge wa majimbo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefikia katika sanduku la kura za maoni, huku mchuano mkali ukitarajiwa Makambako, Iringa Mjini, Kibamba, Namtumbo na Kinondoni. Majimbo hayo ni machache kati ya mengi yanayotarajiwa kuwa na mchuano mkali wa kura za maoni, kutokana na kile kinachoelezwa…

Read More

Huwel aja na gari la ubingwa wa dunia

GARI maalumu kwa ajili ya mashindano ya dunia (World Rally Championship) linatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika raundi ya tatu ya mbio za ubingwa wa Taifa zitakazochezwa Morogoro hivi karibuni. Dereva kutoka Iringa, Ahmed Huwel ndiye ataendesha gari hilo, Toyota GR Yaris ambalo ni ingizo la kisasa zaidi katika raundi hii inayobeba bango la Mkwawa Rally…

Read More

Morocco: Mwanzo mzuri, ila bado tuna kazi

BAADA ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuanza vyema fainali za Ubingwa wa Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), kocha wa kikosi hicho, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amesema huo ni mwanzo tu, ingawa mambo mazuri zaidi yanakuja. Morocco amezungumza hayo baada ya timu hiyo kuanza vyema michuano hiyo kwa kuifunga Burkina…

Read More

Kocha awataja Fei Toto, Kagoma

KOCHA wa Burkina Faso, Issa Balbone amesema viwango vilivyoonyeshwa na nyota wa Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yusuf Kagoma, ndiyo sababu ya kuanza vibaya katika michuano ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN). Timu hiyo ilianza vibaya michuano hiyo baada ya kuchapwa mabao 2-0, katika mechi…

Read More