
Madaktari bingwa wa saratani, wataalamu wa mionzi kukutana Dar kujadili namna ya kudhibiti saratani nchini
MADAKTARI bingwa wa saratani, wataalamu wa tiba mionzi, watafiti, watunga sera pamoja na mashujaa wa saratani kutoka kwenye nchi zaidi ya 20 wanatarajiwa kushiriki kongamano la kwanza la kimataifa la saratani linalotarajiwa kufanyika hapa nchini. Aidha zaidi ya washiriki 600 wakiwemo washirika wa maendeleo, asasi za kiraia na sekta binafsi wanatarajiwa pia kushiriki katika kongamano…