
Kilio cha wananchi kutembea masafa marefu sasa basi, vikianzishwa vituo vipya vya daladala
Unguja. Baada ya wananchi kupaza sauti zao wakilalamikia masafa marefu wanayotembea kwa kukosa vituo vidogo vya daladala kufika katika ya mji, Serikali imeweka vituo vya muda vya kushusha na kupakia wakati ukisubiriwa mpango wa muda mrefu. Katika utaratibu uliokuwapo awali, daladala zilizokuwa zikitoka nje ya mji zilitakiwa kuingia na kushusha kituo kikuu cha daladala Kikwajuni,…